KAMA WEWE NI MPENZI WA UTALII HII NI MUHIMU KWAKO KUHUSU ZANZIBAR



Jambo, Tanzania, leo katika ile sehemu yetu ya ‘JICHO LETU PORINI’ kupitia habarimkusanyiko.blogspot.com tumeona ni vyema tuangazie kuhusiana na Kisiwa cha Zanzibar. Karibuu twende sote.
Zanzibar ni jina la kiarabu-Zenj maana yake nyeusi na Bar maana yake fukwe ya bahari, hivyo muunganiko huo ukaleta maana ya Zanzibar kuwa ni fukwe za watu weusi.

Lakini hapo mwanzo jina ilo lilitumika kama jina linalohusisha takribani fukwe zote zipatikanazo upande wa Afrika mashariki, ikiwa ni pamoja na Kisimayu (Somalia), Beira( Mozambique) baadaye jina la Zenjbar likachanguliwa litumike katika visiwa viwili tu- Unguja na Pemba. Zanzibar imekuwa ikitamkwa tofauti na nchi mbalimbali kama Chancibar, Xengibar, Janjiar n.k

Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Umoja wa Tanzania, jina la Tanzania lilitokana baada ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mnamo mwaka 1964/01/12. Zanzibar ina Serikali na Rais wake. huku ikiwa na makabila makuu mawili ambayo ni Hadimu na Tumbatu na zote huzungumza lugha moja ya Kiswahili.

VIVUTIO VYA UTALII
Kisiwa cha Zanzibar kimekuwa pumziko kubwa sana la wageni kutoka barani Ulaya na nchni Afrika. Ukiwa Zanzibar utapata fursa ya kutembelea mji mkongwe (Stone Town), Visiwa (Mnemba, Chumbe, Changuu, Chapwani, Misali, Bawe, Uzi n.k)

Mbali na vibutio hivyo vingine ni pamoja na nyumba ya Maajabu ( Beit-EL- Ajaab), Msitu wa Jozani, fukwe nzuri na safi za bahari ya Hindi pamoja na mashamba ya karafuu.
Lakini Je wajua kuwa Jumba kongwe kuliko yote Afrika mashariki linapatikana Zanzibar ambalo ni Msikiti uliojengwa mnamo karne ya 11, unapatikana kizimkazi. Pamoja na Jumba la maajab ( Beit-EL-Ajaab) ambalo ni jengo la kwanza Afrika Mashariki kuwa na umeme.

Halikadhalika nyani aina ya Mbega wekundu wanapatikana Zanzibar peke yake katika msitu wa Jozani, lakini mbali na hayo mnamo mwaka 1974 Zanzibar ndio ilikuwa sehemu ya kwanza barani Afrika kuzindua Televisheni ya rangi, huku televisheni ya kwanza ya rangi ilizinduliwa 1964 Tanzania Bara.

Zanzibar ipo umbali wa kilomita 30 toka Tanzania bara kwenye fukwe za bahari ya Hindi.

Hizi ni baadhi ya picha za vivutio vinavyopatikana Zanzibar








ZINGATIA:
Zanzibar ni sehemu yenye tamaduni ya kislamu, hivyo ni vyema ukazingatia mavazi uvaayo ukiwa Zanzibar japo hakuna atakekulazimisha uvae mavazi ya kislamu. Hivyo kwa wanawake hutakiwa kufunika mwili wao na kuvaa gauni au skirts inayovuka magoti yao, pia kwa wanaume kutembea kifua wazi si jambo jema. Hata hivyo, mavaazi ya beach yanarusiwa kuvaliwa ukiwa mazingira husika.

Karibu, Zanzibar!!! Hakuna Matata 
Jicho Letu Porini huandaliwa na Shadrack D. Daniel kutoka Kampuni ya Sam's Car Rental Tours & Safar's  Ltd, ambao ni mabingwa wa kukodisha magari ya aina zote yenye ubora na yaliyokidhi viwango, lakini pia hujishughulisha na uratibu wa safari zote za utalii waweza kuwasiliana nao kupitia www.samscarental.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname