PALE SUMU YA NYOKA INAPOTUMIKA KAMA DAWA




Kuna usemi usemao kuwa 'dawa ya nyoka ni nyoka', lakini hivi karibuni wanasayansi kutoka nchini Uingereza wao pia wamebaini kuwa 'dawa ya nyoka ni nyoka' baada ya kubaini kuwa sumu ya nyoka inapochanganywa na kemikali nyingine huweza kumsaidia mtu aliyegongwa na nyoka.

Kauli hiyo inafuatiwa baada ya wanasayansi hao kusema kwamba wapo katika harakati za kutengeneza dawa itakayowasaidia watu wanaogongwa na nyoka wenye sumu kali, katika nchi za Afrika kusini ya Sahara.

Taarifa zinasema kuwa watafiti katika chuo kikuu cha matibabu ya magonjwa ya nchi za joto cha Liverpool, wapo katika harakati za kukusanya protini kutoka kwenye sumu za nyoka wakali kama 400 na wataongeza kemikali ili dawa iweze kuhimili joto. Huku hadi sasa wakidai kuwa wamekuwa wananyonya sumu ya nyoka kama 80 kila wiki.

Watu wengi ulimwenguni wamekuwa wakikubwa na majanga ya kugongwa na nyoka na inakisiwa kuwa watu 30,000 wanakufa kila mwaka kwa sababu ya kugongwa na nyoka.
Asante sana rafiki kwa kuendelea kuwa na habarimkusanyiko.blogspot.com, tunathamini mchango wako kwetu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname