STAA WA FILAMU AMBAYE AMETANGAZA KUOA NDANI YA MWAKA HUU


Mara zote mwaka unapoanza kila mtu huwa na malengo yake ambayo anakuwa amejiwekea kwa lengo la kuyatimiza pengine ifikapo mwisho wa mwaka na hapa ndipo utasikia plan za watu kama vile za 'kujenga,' 'kununua kiwanja,' 'kununua gari,' 'kuongeza elimu,' 'kupata kazi nzuri' na mambo mengine mengi kama hayo, lakini kwa staa huyu wa filamu Yusuph Mlela yeye anasema ni lazima atimize lengo lake kwa kuoa.

Plan hizo alizisema wakati alipokuwa akizungumza na GPL, ambapo alisema kwamba, baada ya kuishi ‘singo’ kwa muda mrefu, sasa anajipanga kuoa hivyo ndani ya mwaka huu lazima ndoto yake hiyo itimie.

Aidha, Mlela aliongeza kuwa, katika mwaka huu amejiwekea malengo mengi lakini kubwa zaidi ni hilo la kuoa kwani anahisi akiendelea kuwa peke yake kuna mambo atakwama kwa kuwa hatakuwa na mtu wa kumshauri kwa karibu.

Mlela alisema “kiukweli maisha yenyewe ni mafupi na umri nao unaenda hivyo lengo langu kubwa kwa mwaka huu ni kuoa na kuhusu nitamuoa nani itajulikana baadaye lakini kwa sasa tambueni kwamba mwaka huu lazima nioe, nimechoka maisha ya ubachela.”

Hayo ni malengo ya Mlela kwa mwaka huu 2015, lakini nawe pia unaweza kuacha koment yako ukituambia malengo yako kwa mwaka huu na umeanza kuchukua hatua gani kuhakikisha unayafikia msomaji wetu.
  

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname