WATOTO MAPACHA WALIOZALIWA WAKIWA WAMEUNGANA WAPOTEZA MAISHA



Mwanza, Na Goodluck Ngowi
Watoto mapacha waliozaliwa mnamo Januari 3 mwaka huu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mara wakiwa wameungana kuanzia kifua hadi tumbo, wamefariki dunia juzi saa 9.10 alasiri walipokuwa wakisubiria timu ya madaktari kutoka Hospitali ya Rufaa Bugando mkoani Mwanza kuwafanyia upasuaji.

Akizungumza na mwandishi wa blog ya habarimkusanyiko hapo jana, daktari wa wodi ya watoto katika hospitali hiyo, Dk. Shukuru Kibwana, alisema watoto hao walizaliwa na Hellena Paulo (20) mkazi wa Musoma wakiwa na uzito wa kilo 4.6, na walitakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha

Dk. Kibwana alisema timu ya madaktari wa upasuaji na wataalam wengine walifanya kila lililowezekana kuokoa maisha ya pacha hao walioungana, lakini haikuwezekana na kuongeza kuwa kabla ya upasuaji, mapacha hao walitakiwa kupitia tomografia (CT), kufanya kipimo cha ultra sound ili kufahamu endapo watoto hao waliungana baadhi ya maeneo na viungo muhimu.

Hata hivyo, Kibwana alisema watoto hao licha ya kuungana, madaktari bingwa wa hospitali hiyo waligundua viungo vyao vingi vya mwili vilikuwa vikijitegemea, huku kila mmoja akiwa na figo yake, ini na moyo.

Naye muuguzi wa zamu katika wodi ya watoto, Sembosah Hiza, alisema hali ya pacha hao ilianza kubadilika juzi mchana jambo lililokwamisha rufaa yao ya kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi na uchunguzi.

Itakumbukwa kwamba Agosti 6 mwaka jana, mkazi wa Katoro wilayani Geita, Neema Luswetura, alijifungua watoto mapacha wakiwa wameungana sehemu ya kifua na tumbo wakiwa na uzito wa kilo 5.1, hata hivyo walifariki muda mfupi baadaye.

Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname