ODAMA:MWANAUME ATAKAYENIOA ATAMBUE KUWA NAFANYA FILAMU




 Mwigizaji wa filamu za Kibongo nchini Jennifer Kyaka a.k.a‘Odama’, amedai kuwa mwanaume ambaye anaweza kumuoa jambo la kwanza lazima atambue kuwa yeye anafanya filamu kwa muda mrefu hivyo hawezi kuacha kazi yake kwa sababu ya kuingia kwenye ndoa.

Hayo aliyasema Odama alipokuwa akizungumza na paparazi wa GPL, ambapo alidai kuwa haiwezi kutokea kuacha kufanya filamu kwa lengo la kumridhishe mwanaume, huku akidai kuwa maisha yake yamekuwa yakiendeshwa na kazi hiyo kwa muda mrefu.
Picha Odama akiwa na mtoto wake..........


Odama aliongeza kwamba “naamini kuwa yule ambaye atakuja kwa nia ya kunioa kwanza lazima atambue kuwa nafanya filamu, sitahitaji anieleze jambo la kuacha kazi yangu, mimi ni mwanamke ambaye nahitaji kupata maendeleo kupitia kazi zangu,” 
Shukrani kwa kuendelea kutuamini na kuendelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname