FIFA YAIPIGA FAINI KLABU YA SIMBA


Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA limeitaka klabu ya simba kumlipa beki wake wa zamani Donald Mosoti kiasi cha fedha cha taslimu dola elfu kumi na nne na mia nne ambazo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 26,000,000/= ambayo ni fidia ya kuvunja mkataba wake kinyume cha sheria.
Klabu hiyo imetakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 30 baada ya shirikisho hilo kukubaliana na madai yake ya kuvunjiwa mkataba kinyume cha sheria .

Aidha, katika barua hiyo iliyoripotiwa kutumwa kwa klabu hiyo kupitia ofisi za shirikisho la soka nchini TFF imeeleza kuwa endapo Simba itashindwa kulipa fedha hizo ndani ya muda ulioshauriwa suala hili litafikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya Fifa kwa hatua zaidi .

Hata hivyo, Simba iliamua kuachana na beki huyu iliyemsajili toka kwenye klabu ya Gor Mahia ya nchini Kenya katika ya msimu uliopita huku beki huyo akilalamika mkataba wake kuvunjwa bila taratibu kufuatwa.

Beki huyo kwa sasa anachezea klabu ya Tusker ya nchini Kenya baada ya kusajiliwa akiwa amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname