PICHA ZA WEMA NA OMMY DIMPOZI ZALETA MJADALA MTANDAONI


Imeelezwa kuwa huenda kuna project mpya imeanza kutoka kwa msanii wa filamu Wema Sepetu pamoja na yule mkali wa Bongo Fleva Ommy Dimpozi hii ni baada kuposti picha mbalimbali katika mtandao wa INSTAGRAM, huku wakiwa katika pozii tofauti tofauti.

Picha hizo zilipokuwa kila zinapowekwa mtandaoni humo, watu wengi walionekana kubofya kitufe cha kuzipenda, huku wengine wakiacha comment zao kwa kusifia kwa jinsi walivyokuwa wamependeza wawili hao, lakini wengine walienda mbali zaidi na kusema kuwa wamependezana hivyo ingependeza hiyo iwe ni Le PROJECT mupyaaa.

Kama ilivyo kawaida, si kila mtu atakusifu hivyo hivyo pia kulikuwa na baadhi ya watu wakiponda na wengine wakienda mbali zaidi na kuanza kuporomosha lugha chafu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname