HATIMAYE CHAMA PINZANI CHASHIKA DOLA NIGERIA


Hatimaye kiongozi wa wa Chama cha Upinzani cha Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari ameshinda kura za urais na kumuondoa rais aliyeko Goodluck Jonathan madarakani.
Taarifa zinaarifu kuwa tayari rais Goodluck Jonathan amekwisha mpigia simu mpinzani wake Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.

Aidha, Goodluck amekiri kushindwa katika uchaguzi huo ulioshuhudia ushindani mkali

Hii inakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.

Kufuatia matokeo hayo wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa Nigeria sasa inaonekana imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 1960.
Wanaigeria wakionesha furaha yao baada ya matokeo kuanza kutangazwa
Hata hivyo kuliibuka kwa taharuki kubwa haswa baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.

Hali kadhalika Wanigeria wengi wamefurahi kushiriki uchaguzi uliomtoa mamlakani rais Goodluck aliyekuwa hatekelezi wajibu wake kikamilifu.

Pamoja na hayo yote pia taarifa zinaarifu kuwa Buhari bado hajatangazwa rasmi kuwa mshindi na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname