Production Manager wa Kampuni ya marehemu Steven Kanumba 'Kanumba The Great Films' Novatus Mayenja ‘Nova’ amekanusha kuwa kampuni hiyo imefilisika bali imehamishwa kutoka mitaa ya Sinza na kurudishwa nyumbani mitaa ya Kimara Temboni.
“Kampuni ipo kama kawaida isipokuwa tu, utaratibu umebadilika kwa kuhamisha ofisi kutoka ilipokuwa na kuhamishia nyumbani kwa mama Kanumba na kazi zinaendelea kama kawaida,”anasema Nova.
Nova amedai kuwa tatizo lilikuwa ni kodi kwani kodi imekuwa ikipanda kila mwaka hivyo walimudu kulipa kwa miaka miwili kwa pamoja wakaona haina sababu kulipa kodi kubwa bila sababu ya msingi wakati wanaweza kufanya kazi popote.
![]() |
Production Manager wa Kampuni ya marehemu Steven Kanumba 'Kanumba The Great Films' Novatus Mayenja ‘Nova’ |
No comments:
Post a Comment