LOWASSA APEWA ONYO NA JESHI LA POLISI KUHUSU STAILI YAKE YA KAMPENI



Baada ya mgombea urais wa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa kuanzisha staili mpya ya kufanya kampeni zake za kuwatembelea wananchi kwa kutumia usafiri umma na siku ya jana alitembelea soko la Tandale na Tandika na kuzungumza na wafanyabiashara.

Kufuatia staili yake hiyo ya kampeni Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limeibuka na kumtahadharisha mgombea huyo wa urais na kusema kwamba aina hiyo ya kampeni inaweza kutumiwa na maadui wa kisiasa kumdhuru.

Onyo hilo linafuatiwa ikiwa ni siku mbili tangu Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji walipoanza kuwatembelea wananchi kwa kutumia usafiri wa umma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema ziara iliyofanywa jana na mgombea huyo maeneo ya Swahili, Kariakoo ilisababisha mikusanyiko isiyokuwa yalazima na kupelekea shughuli za maendeleo kusimama.

Hata hivyo, wanasiasa wametakiwa kufuata ratiba ya kampeni kwa kuzingatia mwongozo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia Jeshi la Polisi kukabiliana na vitendo viovu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname