MILIONI 6 ZA G. NAKO ZAPOTEA KWENYE KIKAO CHA WASANII!!

Mkali wa muziki wa kizazi kipya kupitia crew ya Weusi G.Nako amejikuta akiuanza mwaka 2016 vibaya baada ya kupoteza pesa nyingi zipatazo dola 3,000 alipokuwa kwenye kikao cha wasanii.

Hayo yamebainika kupitia U Heard ya Januarii 07, 2016 inayofanywa na Soudy Brown kupitia show ya XXL ya Clouds Fm.

Akizungumza na Soudy Brown Baba Levo, ambaye amesema kwamba mazingira yanaonesha G Nako alikaa akiwa amezungukwa na watu wake wa karibu ambao sio rahisi kumwibia G Nako, kwa hiyo huenda pesa hiyo kaangusha.

Hata hivyo, kwa upande wa Nikk wa Pili ambaye ni msemaji wa kundi hilo la Weusi amesema bado hawajajua ni mazingira yapi pesa hizo zimepotea lakini zilikuwa ni dola 3,000 ambazo ni zaidi ya milioni 6.5 kwa pesa ya Kitanzania.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname