BAADA YA KUNGA'AA KWENYE SOKA, HENRY SASA KUWA MCHAMBUZI WA MICHEZO RUNINGANI



Star mkubwa na mkongwe wa soka ulimwengu Thierry Henry ametangaza kustaafu soka na kuanza kujishughulisha na shughuli nyingine.

Henry ni mwanasoka ambaye amekuwa nyota na kuonekana kung’aa kwenye ulimwengu wa soka kwa kipindi cha muda mrefu sana, huku akichezea vilabu mbalimbali ikiwemo Arsenal na Barcelona.

Kufuatia uamuzi wake huo wa kustaafu soka rasmi, Henry amesema kuwa, kuanzia mwakani ataanza kujishughulisha kama Balozi wa ‘Sky Sports’ huku akisema kuwa anajisikia furaha kuchezea vilabu vikubwa na pia anaamini anajiunga na kituo kikubwa cha Television na matarajio yake ni kuwa mchambuzi bora wa michezo kwenye kituo hicho.





No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname