Diamond hakamatiki, achukuwa tuzo kama zake channel O



Mwanamuziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, amefanikiwa kunyakua tuzo tatu za Channel O.

Mwanamziki huyo ameishangaza Afrika baada ya kunyakua tuzo kubwa ya Video Bora ya mwaka na kuwa msanii aliyeondoka na tuzo nyingi, huku akiondoka na tuzo ya msanii bora Afrika Mashariki na mwanamuziki bora anayechipukia.
Aidha, Diamond amesema kuwa pamoja na kuwashinda wasanii mahiri barani Afrika, lakini bado anahisi hajafikia hatua anayostahili na kwamba anahangaika kuhakikisha anaifikia na kuendelea kukaa juu siku zote.

“Nafahamu kuwa bado nina kazi kubwa kuhakikisha nafikia hatua ambayo naiota, najua kwamba nina kazi kubwa kuhakikisha nafika huko ila sitokata tamaa na bado natakiwa kuendelea kusimama katika nafasi niliyopo.

Mbali na hayo, Diamond alisema kuwa bado anatambua kuwa anadeni kubwa kwa Watanzania na anahitaji kupata tuzo nyingi zaidi zikiwamo za BET na nyinginezo.

Nyota huyo aliyempiku mwanamuziki maarufu barani Afrika, Davido, amesema anamshukuru sana Mungu na mashabiki wake waliompigia kura na kusema anaamini bila wao asingeweza kufikia hapo mafanikio hayo.
Safari hii davido ashindwa kufurukuta mbele ya Daimond Platnumz

“Kiukweli, haikuwa rahisi kabisa, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kuungwa mkono na mashabiki, vyombo vya habari ndani na nje ya nchi iliwezesha Bongo Fleva yetu kuandika historia mpya kwenye ramani ya muziki wa Afrika,” alisema Diamond

Hali kadhalika msanii huyo ameongeza kuwa kufanikiwa kwake inaonyesha ni jinsi gani umoja ni nguvu, pia inadhihirisha kuwa muziki wetu ukipewa sapoti na kipaumbele unaweza kufika mbali zaidi.


Afrika ilishuhudia Diamond akinyakua tuzo hizo na kumpiku Davido ambaye alikuwa akiwania vipengele vitano, huku mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest naye akinyakua tuzo tatu.

Wasanii wengine waliochukua tuzo hizo ni pamoja na Tiwa Savage, DJ Clock, K.O, Riky Rick, Burna Boy, Emmy Gee pamoja na Prince of Hip Hop.
Naye mwanamuziki Kcee alisema, Diamond ni kati ya wasanii wanaoibukia Afrika wenye vipaji na watakaoweza kuitangaza Afrika hapo baadaye.
“Napenda nikimwona anafanya shoo, ni kati ya wasanii wenye vipaji wanaoibuka hivi sasa na anavyoonekana ni kwamba hachoki na kile anachokifanya. Tulimwona alipotoa ‘Number One’, wengi walidhani alibebwa na Davido, lakini ameonyesha kwamba anaweza baada ya kutoa ‘Mdogo Mdogo’ na video yake mpya (akimaanisha ‘Ntampata Wapi’),” alisema Kcee.

Kcee aliyenyakua tuzo ya wimbo wa kushirikiana kupitia wimbo wake ‘Pull Over’, huku Tiwa Savage akifanikiwa kushinda tuzo kupitia wimbo wake wa ‘Eminado’.

Kwa habari za burudani pia tembelea habarimkusanyiko.blogspot.com kwani tupo vizuri, tafadhali endelea kuungana nasi kila siku

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname