DIAMOND:NILITAMANI KUWA NA MTOTO, LAKINI WANAWAKE ZANGU HAWAKUWA TAYARI KUNIZALIA



Msanii wa muziki Nasibu Abduli aka Diamond Platnumz amesema kuwa wapenzi wake wote aliowahi kutoka nao hawakuwa tayari kuzaa watoto jambo linalomfanya hadi leo kukosa mtoto, licha ya yeye kupenda kuwa na watoto.

Akizungumza kwenye kipindi cha Live Chumba cha Habari kinachorushwa na Global TV online, Diamond alieleza jinsi wapenzi wake wazamani ambao ni Mwigizaji Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na matangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’ kuwa wote hawakuwa real kuzaa hivyo walikuwa wanachengachenga.

Hayo yote yalifuatiwa mara baada ya Diamond kuulizwa kwamba amekuwa akitangaza kupenda watoto lakini kwa nini hana mototo hata wa dawa licha ya kuwa na uhusiano na wanawake tofauti tofauti.

“Ni kweli napenda watoto lakini siwezi kupata mtoto peke yangu bila mwenzangu. Lazima kuwe na mwenzangu ambaye tutakubaliana. Nilichojifunza ni kwamba wenzangu hawakuwa real (hawakumaanisha) hivyo wakawa wanachengachenga.”

Hata hivyo Diamond aliendelea kueleza kuwa mwanadada Penny aliwahi kupata ujauzito wake mara mbili.

“Ukweli Penny ningezaa naye, aliwahi kuniambia ana mimba yangu, sikuamini, nikampeleka hospitali kupima ikawa kweli. Kesho yake nikamnunulia gari, nikamwambia mama tulia. Siku mbili tatu akasema mimba imetoka”

Diamond aliendelea kusema kwamba “Nikaja nikamjaza kingine cha pili (mimba), nayo baada ya muda akaja kuniambia imetoka. Nikaona huyu mzinguaji, nikammwaga. Lakini iliniuma sana.

Mbali na Penny Diamond alisema kuwa “Kwa wengine (Jokate na Wema) walikuwa wakinichenga tu bila sababu, unamuona huyu hataki kubeba mimba yangu. mtu kwa mdomo anasema kwamba yuko na wewe kikamilifu lakini kwa matendo unaona siye.

Pamoja na hayo, Diamond alibainisha kuwa ni ukweli usiopingika kweli anatamani kabisa kuwa na mtoto.na alipoulizwa kati ya wanawake hao wote ni yupi alitarajia kumuoa Diamond alijibu “Ah! Siwezi kumsema hapa” 

Ni haki yako kupata habari mbalimbali kutoka habarimkusanyiko.blogspot.com, asante kwa kuwa nasi

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname