BEI YA FILAMU ZA KIBONGO KUSHUKA MWAKANI

Baada ya kipindi kirefu wasanii wa filamu kulalamika kuhusu baadhi ya watu kuzikopi kazi zao na kuziuza kwa bei ya kutupa hadi kufikia shilingi 1000 na wengine 500, hii leo Disemba 18 Kampuni ya Steps Entertainment, wameamua kutambulisha bei mpya na muonekano mpya wa DVD covers za filamu zao kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wasanii hao akiwemo Jacob Steven JB, King Majuto wameseama kuanzia mwezi wa pili mwakani CD moja itauzwa shilingi 1500 kwa bei ya rejareja badala ya shilingi 3000 iliyopo kwa hivi sasa.

Hata huvyo, wasanii hao wameazimia kuendeleza harakati za kupambana na wezi wa kazi zao.

Wakati hayo yakiendelea muigizaji Jackline Masawe “Wolper”na King Majuto wameonekana wakiwa mzigoni wakitengeneza filamu yao mpya. Ingawaje bado jina la movie halijawekwa hadharani, pamoja na lini movie hiyo itatoka, mashabiki wengi mitandaoni wameonesha kutegemea kazi nzuri kutoka kwa waigizaji hao wenye uwezo na uzoefu mkubwa.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname