MUIGIZAJI JOHARI ASEMA KIZAZI CHAKE KIPO IMARA




Mwigizaji nguli wa filamu hapa nchini, Blandina Chagula "Johari" amekanusha tetesi na uvumi kuwa yeye anamatatizo ya kizazi na hivyo hawezi kushika ujauzito na badala yake amesema kuwa kizazi chake kipo imara.

Johari amesema kwamba kizazi chake kinafanya kazi na anachosubiri ni kumpata mwanaume ambaye atakuwa tayari kumuoa ndipo atakaporuhusu kuzalishwa.

Akizungumza hivi karibuni Johari alisema kuwa, endapo ikitokea tayari yupo ndani ya ndoa anaweza kufanya hivyo, lakini kwa maneno ya watu kamwe watasubiri kwani anaamini kizazi chake kipo imara na wakati wowote akiamua kushika mimba kitafanya kazi.

“Kizazi changu kinafanya kazi na mipango hiyo ya kushika mimba mimi siwezi kukubali nipate mtoto kabla ya kuolewa, suala la kufanya jambo kwa lengo la kuwafurahisha watu mimi siwezi kufanya hivyo,” alisema Johari.


Ni haki yako kupata habari zote zinazotufikia kutoka kwetu, tafadhali endelea kuwa nasi tupo kwaajili yako msomaji wetu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname