HII NI MAHUSUSI KWA WEWE MPENZI WA SOKA



Zikiwa zimesalia takriban wiki tano ilikuanza rasmi kwa michuano ya kombe la Afrika, huko Equatorial Guinea ambao ni wenyeji wa mashindano hayo, taarifa ni kwamba maandalizi yamepamba moto ambapo viwanja viwili tu ndio viko tayari kati ya vinne vitakavyotumika katika michuano hiyo.

Viwanja vilivyokamilika ni katika mji mkuu wa Malabo na Bata ambao ni mji wa pili kwa ukubwa.

Taarifa zinaeleza kwamba imekuwa ngumu kujenga viwanja vingine kuanzia mwanzo katika majimbo ya Mongomo na Ebebiyin, kaskazini mwa nchi hiyo.

Wakandarasi wamepewa sehemu mbalimbali kukamilisha kazi ya ujenzi kama vile vyoo, bafu, milango pamoja na mapaa. Hata hivyo kazi hiyo inaonekana kuendelea polepole

Sambamba na hayo, kumekuwa na wasiwasi kwa uwanja wa Mongomo wenye uwezo wa kuchukua watu 10,000, kama utakuwa tayari kwa muda wa kuanza kwa michuano ya kombe la Afrika.

Vigogo kumi na sita wa soka barani Afrika wakiongozwa na mwenyeji Equatorial Guinea wanatarajia kuchuana kuwania ubigwa wa Afrika kuanzia January 17.

Itakumbukwa kwamba Morocco ilijitoa kama mwenyeji kwa kile kilichodaiwa kuwa ni hofu ya ugonjwa wa Ebola kufika nchini humo.

Ni wajibu wetu kuhakikisha unapata kila taarifa kutoka kwetu, asante kwa kuwa nasi

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname