USHAWAHI KUKUTANA NA BAISKELI ILIYOTENGENEZWA KWA DHAHABU, KAMA BADO HEBU ANGALIA HAPA



Hii nayo ni kali ya mwaka baada ya Kampuni ya Goldgenie kuamua kutengeneza baiskeli kwa dhahabu ambayo itakuwa karibu kila sehemu ya baiskeli hiyo.

Wataalam wa kampuni hiyo ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hiyo, ambapo kuanzia mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kutembea pamoja na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu.

Mkurugenzi wa kampuni iliyotengeza baiskeli hiyo anasema inaweza kuendeshwa barabarani kama ilivyo kwa baiskeli nyinginezo

Hata hiyo, bado haijafahamika kwa sasa ni idadi kiasi gani za baiskeli hizo zitakazotengezwa, lakini ikiwa utakuwa na bahati sana unaweza kupata moja kama hiyo. Lakini itakubidi ununue kufuli kuifungia baiskeli yako ikiwa hautakuwepo sehemu ambako umeiwacha.

Baiskeli hiyo mpya iliyotengezwa kwa dhahabu tayari imezinduliwa na bei yake? Pauni laki mbili na hamsini, Bei hii ni ghali hata kuliko bei ya gari jipya la Ferari.

Huu ndio muonekano wa baiskeli hiyo....


Hata sehemu zake za kubadilishia gia ni dhahabu tupu.

Spoko zake pia ni dhahabu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname