WANAWAKE WAILALAMIKIA SERIKALI YAO KWA KUWAFUNGA KIZAZI



Baada ya hivi karibuni kuzuka kwa mijadala nchini Kenya endapo ni haki kuwafunga kizazi wanawake wenye ulemavu wa akili . Sasa hiki ndicho kilichoibuka tena baada ya wanawake nchini humo kufanya maandamano ya amani mjini Naiirobi, huku wakidai kuwa walifungwa kizazi kwa lazima kutokana na hali yao ya HIV

Kikundi cha wanawake wenye virusi vya Ukimwi nchini Kenya, kimewasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali, huku kikiituhumu kwa kuwapangia wafungwe kizazi kwa lazima kutokana na hali zao za kiafya.

Inaelezwa kuwa ni kwa mara ya kwanza kundi la kina mama kujitokeza na kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali, wakidai kuwa wao walishurutishwa kufunga uzazi na baadhi yao wakifanyiwa upasuaji huo hata bila ufahamu wao.

Akina mama hao ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi wanasema mpango huo unaoendeshwa na serikali kupitia Wizara ya Afya na mashirika mengine unakiuka katiba ya nchi, na hivyo wanataka kulipwa fidia na pia serikali kuharamisha mpango huo mbali na kuweka sera mpya kuhusu mpango wa kufunga uzazi.

Taarifa zinaarifu kuwa katika maandamano yao wanawake hao walivalia mavazi yenye maandishi yasemayo ''koma mpango wa kulazimisha kina mama wanaoishi na virusi vya ukimwi, kufunga uzazi, ''

Naye Allan Malechi, ambaye ni wakili wa kina mama hao, anasema kuwa idadi ya wanawake hao waliofanyiwa upasuaji wa kufunga uzazi bila idhini yao huenda ikaongezeka zaidi kwa kuwa kuna ripoti kuwa mradi huo unaendelea katika sehemu nyingine.

Pamoja na hayo, wanaharakati hao wamesema kuwa mradi huo ni sawa na ukatili wa kibinadam na kutaka serikali kupitia kwa Wizara ya Afya kutoa taarifa rasmi, Lakini pia wanawake hao wameitaka serikali iwalipe fidia kwa oparesheni walizofanyiwa kinyume na matakwa yao

Kesi za namna hii zimewahi kuwasilishwa mahakamani katika mataifa kadhaa ya Afrika ikiwamo Mahakama ya nchini Botswana mnamo mwaka 2012, ambapo iliamua kuwa wanawake watatu wanaoishi na virusi vya Ukimwi, waliofungwa kizazi kwa kulazimishwa walipwe fidia na serikali.

Lengo la habarimkusanyiko.blogspot.com ni kuhakikisha hupitwi na taarifa yoyote ulimwenguni, asante kwa kutuchagua na endelea kuwa nasi kila siku.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname