MFAHAMU MSANII WA FILAMU MWENYE WATOTO WENGI KULIKO WOTE TANZANIA



Mwigizaji na mwongozaji mahiri wa filamu za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, ameweka bayana kuhusu idadi ya watoto wake na kusema kuwa anawatoto wanane tu. Huku akikanusha vikali kuwa na timu ya mpira (watoto 11) idadi inayovumishwa na baadhi ya watu wengi.

Hata hivyo, Dude anatajwa kuwa ni msanii anayeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto kwa upande wa wasanii wengine wa kiume hapa nchini Tanzania.

“Kila mtu anasema anavyojisikia, mara ooh! Dude ana timu nzima ya mpira wa miguu, lakini ukweli ni kwamba nina watoto wanane tu, ambao nimezaa na wanawake wanne,” alisema.
Msanii Kulwa Kikumba "Dude"
Aidha, Dude aliendelea kusema kwamba “Kwangu naona si haba maana kuna watu ambao hatujui kama wana majukumu, kila siku wanajiona watoto wanayakimbia majukumu yao, mimi sipo hivyo.”

Pamoja na hayo, Dude aliongeza kuwa anawapenda watoto wake na ndio maana kila mmoja wao alipozaliwa na kubainika ni wake, alianza mara moja kutoa huduma na kumtambulisha kwa familia yake.

“Unajua wapo wasanii wengi tu wenye watoto, lakini wengine hukimbia majukumu kwani wanataka kila siku kula starehe na mizigo kuwaachia waliozaa nao,” aliongeza msanii huyo

Shukrani kwako kwa kuendelea kuwa nasi kupitia blog hii ya habarimkusanyiko.blogspot.com, tunaahidi kuendelea kuwa karibu nawe kwa kukuletea habari mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname