HII NI MAALUM KWAKO WEWE UNAYEPENDA KUPIKA


Karibu mpenzi msomaji katika safu yetu mpya ya mapishi, leo katika mapishi tunakuletea pishi la wali wa mbogamboga yaani vegetable rice, chakula hiki huliwa na watu wa aina zote, yafuatayo ni mahitaji yatakayo kamilisha pishi letu la leo…

MAHITAJI

  •  Mchele
  •  Mafuta
  •  Karoti
  •  Zuchini (baby maro)
  • Njengere
  • Viazi
  • Chumvi

JINSI YA KUANDAA

  •  Hizo mbogamboga utazikata mkato wa “Cubes” ispokuwa kitunguu peke yake chenyewe utakikata kwa kukichop yaani ukishakikata kitunguu unakipondaponda na kisu ili kisagike na kuwa chembe chembe ndogo sana.
  •  Zingatia kwamba katika mbogamboga zote zuchini haimenywi, ipo mfano wa tango, na wingi wa mbogamboga utategemea sana na kiasi chako cha mchele.
  • Pia hakikisha mchele wako umeloana vizur, huku maji yako ya moto yakiwa pembeni kwa ajili ya wali kwani utahitajika kupika kwa mtindo wa kukaanga.

JINSI YA KUPIKA

  • Weka sufuria jikon i kisha mimina mafuta kiasi na usubiri t=yapate moto vizuri na uweka vitunguu mpaka vibadilike rangi na kuwa vya rangi ya kahawia/ brown.
  • Baada ya hapo weka mchele wako na chumvi kiasi, kisha weka zile mbogamboga zako na yale maji ya moto uliyokuwa umeyaweka pembeni hapo awali, lakini pia unaweza kutumia kitunguu swaumu na nazi kwa kuongeza ladha ya chakula chako kama utapenda.
  • Maji yakishakauka utafunika wali wako na utawekea moto juu na chini kwa maana hiyo zile mbogamboga zitaiva katika hatua hii ya mwisho.

Hadi kufikia hapo pishi letu litakuwa limeamilika na lipo tayari kwa kupakuliwa na unaweza kula na mboga yoyote unayoipenda, lakini hupendeza zaidi mboga hiyo ikiwa ni ya mchuzi. 

Pishi hili limeandaliwa nakuletwa kwenu na Asha Habibu.

Lengo letu ni kumgusa kila msomaji wetu katika nyanja tofauti tofauti, hivyo tunakusihi endelea kuungana nasi kila siku kwa vitu vizuri zaidi

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname