MBUNGE AWATUHUMU WABUNGE WENZAKE KUWA WALIJARIBU KUMVUA NGUO


Mbunge wa eneo la bunge la Mbita nchini Kenya Millie Odhiambo aliyedai kuwa wabunge wenzake walijaribu kumvua nguo wakati walipokuwa wakipinga mswada wa usalama
Kufuatia vurugu na purukushani zilizoonekana katika bunge la Kenya wakati wa kupitishwa kwa mswada wa usalama, mbunge mmoja mwanamke sasa amejitokeza na kudai kwamba wabunge wenzake watatu wanaume walijaribu kumvua nguo.

Mbunge huyo Millie Odhiambo aliandika katika mtandao wake wa facebook kwamba wabunge wengi walipigwa, huku yeye akidai kupigwa ngumi machoni na mbunge mmoja kabla ya wabunge wawili kujaribu kumvua nguo.

Hivi ndivyo ujumbe huo ulivyosoma katika mtandao wake wa facebook:

''Tulijaribu kulemaza kikao hicho asubuhi yote.lakini ilipofika mwendo wa saa nane waliwasili wakiwa wamejitayarisha ya kutosha.Wabunge wengi walipigwa.Mimi mwenyewe nilipigwa ngumi machoni na mbunge mmoja huku wengine wawili wakijaribu kunivua nguo.lakini mimi si wa kulia lia kwamba nimepigwa kofi! Mbunge aliyenipiga amejua kwamba mimi ni mbunge wa Mbita aliyechaguliwa na wala si kuteuliwa.Walipojaribu kunivua nguo mimi mwenyewe niliwamalizia kuwavulia nguo.Mimi siogopi na nashkuru nilivyoumbwa.Sitakubali kutishwa kwa kutumia jinsia yangu'',aliandika bi Millie..

Maandishi hayo baadaye yalifuatiwa na mengine yaliyosomaka kuwa ameenda kupigwa picha na kuangaliwa jicho lake hospitali.


No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname