NDEGE ILIYOPOTEA YAENDELEA KUTAFUTWA




Zoezi la kuitafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili linaeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.

Ndege hiyo iliyokuwa na watu 162 wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini ikielekea nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia.

Taarifa zinasema kwamba shughuli za utafutaji wa ndege hiyo zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.

Aidha, ndege za kijeshi kutoka nchini Indonesia na Singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo iNlitoweka.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname