Kufuatia kupotea kwa ndege ya Shirika la Air Asia wanamaji kutoka nchini Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu Jumapili katika Bahari ya Indonesi.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today ikiwa ni siku ya tatu sasa tangu kuanza msako dhidi ya ndege hiyo.
Aidha, idadi ya wataalam wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia, Australia, Korea Kusini, Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo.

No comments:
Post a Comment