MARUBANI WANOGEWA NA LIKIZO YA SIKUKU YA KRISMASI NA KUSABABISHA SAFARI ZA NDEGE KUKWAMA


 EMEELEZWA kuwa zaidi ya abiria mia moja wa ndege ya Air Tanzania wamekwama, baada ya safari za shirika hilo la ndege kuarishwa.

Taarifa zinasema kuwa wengi wa abiria hao walikuwa wakifanya safari kuelekea nchini Comoros na wengine wakiwa katika safari za ndani, wakielekea Mtwara na Kigoma, wamekwama kwa siku mbili mjini Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na kadhia hiyo shirika hilo lililazimika kukodi hoteli kuwahifadhi abiria hao kama ilivyo ada inapotokea dharura wakisubiri muafaka wa namna watakavyosafiri kuelekea Comoro.

Hata hivyo, baadhi ya abiria hao akiwemo Sharifu Hashim, Balozi wa heshima wa Comoro huko Chicago nchini Marekani, alisema mambo yake mengi yamekwama kutokana na tukio hilo na hajapata uhakika ataondoka lini.

Zenabal Mwarabu yeye hofu yake ni kwa namna gani ataweza kuiwahi ndege aliyokuwa aunganishe Kisiwani Comoro kuelekea katika kisiwa kingine cha Rarinyo. Msawi Seifu anasema ijapokuwa tatizo hili limetokea lakini Air Tanzania ni mkombozi kwa wana Comoro.

Pamoja na hayo, Lily Fungamtama, Mkuu wa Kitengo cha Biashara amesema tayari Air Tanzania inashughulika kuhakikisha abiria wote wanasafiri mapema kesho.

Sambamba na hayo, inaelezwa kuwa sikukuu za mwisho wa mwaka ndilo tatizo la kukwama kwa abiria hao, kwani marubani hawajarejea kazini tangu walipoondoka, na walitegemewa kurejea kazini tarehe 27 mwezi huu, baada ya sherehe za Christimas, lakini haikuwa hivyo na kusababisha sinto fahamu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname