KOCHA PATRIC PHIRI AMESEMA AMEARIFIWA KUHUSIANA NA KIBARUA CHAKE KUSITISHWA


Kocha Patrick Phiri akitoa maelekezo kwa kikosi cha timu ya simba kipindi alipokuwa akiifunza kikosi hicho

Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa. 

Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.

"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.

"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.

Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.

"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname