Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameombwa kutengua uteuzi wa mawaziri, mwanasheria mkuu na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini waliotajwa kuhusika katika ufisadi wa mabilioni ya fedha kutoka katika akaunti ya Escrow.
Akizungumza na wanahabari hivi karibuni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu nchini (OJADACT) Edwin Soko, alisema anamuomba rais kutengua uteuzi wao kwa kutumia ibara ya 36 (2) na kuteua wengine.
“OJADACT tunamuomba Rais kutowaonea aibu waziri wa nishati na madini Prof, Sospeter Muhongo, Waziri wa Ardhi na Makazi Prof, Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu Fredrick Werema na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi kwa kutengua uteuzi wake kwa kutumia ibara ya 36(2) na kuteua wengine”, Alisema Soko
Mbali na hayo, OJADACT iliwapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri waliofanya ya kufichua ukweli wa sakata hilo pamoja na wabunge wote waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania maslahi ya taifa
wakiongozwa na mbunge wa Kigoma kusini, David Kafulia.
“tunawapongeza sana wanahabari kwa kuwafichua mafisadi, licha ya
baadhi yao kutaka kufunika kombe mwanaharamu apite pamoja na wabunge wote waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania maslahi ya taifa wakiongozwa na David Kafulila”, Alisema Soko
Sambamba na hayo, chama hicho kilimwomba Waziri wa Fedha kusimami kauli yake ya kuwataka wote waliopata mgao huo wa fedha za Escrow kulipa kodi kama alivyotangaza bungeni.
Habarimkusanyiko.blogspot.com ipo kwa ajili yako tafadhali endelea kuungana nasi kwa habari zaidi kila iitwapo leo .
No comments:
Post a Comment