VIJANA WAASWA KUACHA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA


Vijana wameaswa kuachana na tabia ya kutumia madawa ya kulevya kwani matumizi hayo hupekea mabadiliko ya hisia na ufahamu wa akili zao.

Hayo yamebainisha Disemba 14 na mkurugenzi wa Drugs corner Solution (mtandao wa marafiki wa kupinga vita dawa za kulevya) Bw, Iman Andrew, wakati akiongea na na waandishi wa habari ofisini kwake nakusema kuwa vijana wanatakiwa kuepukana na vipumbaza, vichangamsho, vileta njozi pamoja na viyeyushi, kwani hupelekea kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa ufahamu kupungua na kufanya matendo yasiyo ya busara katika jamii.

Aidha amesema kuwa matumizi ya dawa za kulevya yanaathari kubwa, ikiwa ni pamoja na kupunguza nguvu kazi kwenye familia, ugomvi, mauaji ya kikatili, kushindwa kutunza familia jambo ambalo huchangia sana kushuka kwa nguvu kazi ya taifa.

Mbali na hayo, Adrew alioneza kuwa vijana wanapaswa kutambua kuwa serikali inatambua uwepo wa vijana kwa kuhakikisha kuwa asilimia kumi (10%) ya mapato ya jiji inayokusanywa katika kodi inakusudia kusaidia vijana na kuwataka vijana kila mmoja kuwa na bima ya afya itakayowasaidia katika masuala ya matibabu.

Pamoja na hayo, Mkurugenzi huyo alibainisha sababu zinazopelekea watu wengi kushindwa kuacha madawa ambapo amesema kwamba, sababu kubwa inayopelekea watu wengi kushindwa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya ni kuwepo kwa utegemezi mwilini hatimaye mwili kushindwa kufanya kazi zake pale anapokosa dawa za kulevya.

Story hii imeandaliwa na Theo M. George ambaye ni mwakilishi wa habarimkusanyiko.blogspot.com kutoka mkoani Arusha

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname