VIJANA WASHAURIWA KUACHA KUTEGEMEA KUAJIRIWA




 Arusha, Theo.M.George 
Vijana vya vyuo vikuu vya Jumuiya ya Afrika mashariki washauriwa kuachana na mitazamo potofu kwa kuitegemea serikali kuwaajiri na badala yake wanapaswa kuangalia njia mbadala yakuweza kujiajiri wao wenyewe kwa kuanzisha miradi mbalimbali itakayo wasaidia kujiendeleza kimaisha.

Hayo yalisemwa na Katibu wa Wizara ya vijana kutoka Kigali nchini Rwanda, Rosemary Mbabazi katika mkutano wa vijana wa Afrika Mashariki ulioanza Disemba 5 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha.

Mbabazi alisema kuwa, vijana wengi wamekuwa wakiitegemea serikali kuwapatia ajira mara tu baada ya kumaliza masomo yao, jambo linapelekea vijana wengi kuishia kuilaumu serikali pindi wanapokosa nafasi hizo za ajira na hatimaye wengine kukata tamaa kabisa.

Mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa kutoka nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki na wanafunzi wa vyuo vya Afrika Mashariki ulinuia kutoa elimu kwa vijana jinsi ya kutatua matatizo yanayo wakabili, pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha katika maisha yao kila siku.

Naye afisa mkuu Prof Nuhu Hatibu wa Kilimo Trust kutoka Kampala nchini Uganda alisema kwamba "baadhi ya changamoto zinazo wakabili vijana ni kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuwepo kwa ongezeko kubwa la virusi vya Ukimwi,(HIV/AIDS) jambo linaloathiri vijana kwa kiasi kikubwa katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki"

Afisa huyo aliongeza kusema kuwa, vijana wanatakiwa kutambua kuwa kilimo ni moja ya njia ambayo inaweza kuwakwamua kiuchumi kwa kufuata taratibu za kilim,  ikiwa ni pamoja na vitendea kazi kama upatikanaji wa trekta ,plau, sambamba na mbolea itakayo saidia katika kilimo

Sambambana na hayo mkutano huo iliongozwa na  kaulimbiu isemayo  "Kijana. fikiria,Ongea na Shiriki (Youth.Think,Speak,Participate)’’

Unastahili kupata habari zote hizi kila kona ya Tanzania, tafadhali endelea kuungana nasi kila. siku 

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname