AAM PICTURE KAMPUNI MPYA YENYE MALENGO YA KULETA MAPINDUZI KATIKA TASNIA YA MOVIE BONGO

Hii ndiyo filamu ya kwanza itakayoanza kutoka katika Kampuni ya AAM PICTURE

Ni wazi kwamba tasni ya filamu nchini imekuwapo kwa miaka kadhaa sasa na imekuwa ikiendelea kufanya vizuri, licha ya kuwepo kwa mapungufu machache katika tasnia hiyo yakiwemo yale ya ubora hafifu wa kazi hizo.


Hivyo kwa kulitambua na kuliona hilo Kampuni mpya kabisa inayokwenda kwa jina la AAM PICTURE imedhamilia kufanya maboresho hayo machache ambayo yamekuwa yakijitokeza katika baadhi ya movie zetu za kibongo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanatoa filamu zitakazokuwa na ubora wa kutosha katika masuala ya picha  pamoja na uongozaji pia.

Kampuni hiyo yenye Makao yake Makuu Ukongo, Mongolandege jijini Dar es Salaam inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu aitwaye Juma Dede yeye anasema kuwa kwa kuanzia wataanza na filamu yao inayokwenda kwa jina la 'Night Dreams' filamu ambayo amesema wanamatarajio makubwa kuwa itafanya vizuri kwa umma wa Watanzania kwani imesheheni kila aina ya mikasa humo ndani.

Hata hivyo, Dede alifafanua kuwa filamu hiyo kwa sasa imeshaanza kufanyika na ni vipande vichache (scene) tu ndizo zimebaki na zinaendelewa kufanyiwa kazi ili kuikamirisha kabisa filamu hiyo.

Aidha, Dede amewasihi Watanzania na wapenzi wakutazama filamu za hapa nchini kuisubiri kwa hamu filamu hiyo kwani itawaburudisha na kuwapatia mafunzo pia ya kimaisha.

Msomaji wa blog hii ya habarimkusanyiko.blogspot.com tafadhali endelea kuungana nasi na nipo tayari kuanza kukupatia baadhi ya vipande vya filamu hiyo kuanzia hivi karibuni ili uweze kuanza kuona nusu ya uhondo utakaopatikana kupitia filamu hiyo ya 'Night Dreams' kazi iliyofanywa na Kampuni ya AAM PICTURE

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname