HIKI NDICHO ALICHOKISEMA LUNDENGA BAADA YA BASATA KUFUNGA MASHINDANO YA MISS TANZANIA



Mkurugenzi wa kampuni ya  Lino International, Hashim Lundenga
Baada ya siku kadhaa kupita tangu Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kuifungia Kampuni ya Lino International kuendesha mashindano ya ulimbwende maarufu kama Miss Tanzania kwa miaka miwili, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Hashim Lundenga amesema hatua hiyo inatokana na baadhi ya watu wachache wenye lengo la kuhakikisha Miss Tanzania inapotea kwenye ramani ya burudani.

Lundenga aliendelea kusema kwamba yote hayo ni kutokana na shinikizo kutoka kwa baadhi ya watu wenye dhamira ya kuitoa kwenye mstari wa mafanikio sanaa ya urembo nchini.

Asante kwa kuendelea kuungana nasi katika kupashana habari, tafadhali endelea kutembelea blog hii mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname