PAPA FRANCIS ATEUA MAKADINALI WAPYA



 
Papa Francis
Papa Francis amewachagua makadinali 20 wapya akiwemo kutoka mataifa ya Tonga, Ethiopia na Myanmar.

Katika uteuzi huo kumi na tano kati yao wako chini ya umri wa miaka 80 swala linalowafanya kuingia katika mkutano wa faragha ili kumchagua atakaye mrithi papa.

Aidha, Papa Francis amesema kuwa uteuzi wa makadinali hao kutoka mataifa 14 kutoka kila bara duniani unaonesha kuwapo na uhusiano wa karibu wa Vatican na makanisa ya kikatoliki kote duniani.

Makadinali hao wanatarajiwa kuapishwa rasmi February 14 mwaka huu, huku papa Francis pia akiwa ametangaza kuwa siku ya Jumapili atazungumza na makadinali wote ili kujadiliana kuhusu usimamizi wa kanisa hilo huko Vatican mnamo tarehe 12,13 mwezi Februari.

Orodha ya Makadinali hao wapya ni hii hapa ifuatayo:

Manuel Jose Macario do Nascimento Clemente (portugal)

Berhaneyesus Demerew Souraphiel (Ethiopia)

John Atcherley Dew (New Zealand)

Edoardo Menichelli (Italy)

Pierre Nguyen Van Nhon (Vietnam)

Alberto Suarez Inda (Mexico)

Charles Maung Bo (Myanmar)

Francis Xavier Kriengsak Kovithavanij (Thailand)

Francesco Montenegro (Italy).

Daniel Fernando Sturla Berhouet (Uruguay)

Ricardo Blazquez Perez (Spain).

Luis Lacunza Maestrojuan (Panama)

Arlindo Gomes Furtado, (Capo Verde).

Soane Patita Paini Mafia (Tonga)

Jose de Jesus Pimiento Rodríguez (Colombia)*

Luigi De Magistris (Italy)*

Karl-Joseph Rauber (Germany)*

Luis Hector Villalba (Argentina)*

Julio Duarte Langa (Mozambique)

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname