KAMA ULIKUWA HUJUI KUWA KITUNGUU SWAUMU NI DAWA FANYA UKUTANE NA DK MANDAI HAPA AKIELEZA ZAIDI


Kuna baadhi ya vitu huwa tunavitumia, lakini wengi wetu huwa hatufahamu undani wa umuhimu wa vitu hivyo, hapa leo nakukutanisha na mtaalam wa tiba mbadala hapa nchini Dk Abdallah Mandai kutoka kituo cha Mandai Herbalist Clinic, ambaye anaelezea namna kitunguu swaumu kinavyoweza kutumika kama suluhisho la baadhi ya matatizo yetu kiafya.


Dk Mandai anasema, kitunguu swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongeza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali, lakini wakati kiungo hicho kikitegemewa katika kuonogesha vyakula wataalam wa tiba asili wanasema ni kiungo hicho ni dawa endapo kitatumika vizuri.

Mtaalam huyo anaeleza kwamba, baadhi ya magonjwa ambayo yanayoweza kutibika kwa kutumia kitunguu swaumu ni pamoja na ugonjwa wa kifua, au mkamba, ambapo anasema kuwa, ugonjwa huo ambao hujitokeza baada ya mifereji inayoingiza hewa mapafuni kupata maambukizi na kusababisha mgonjwa wa kukohoa na huwa kikohozi chenye sauti mara kwa mara, huku kikiambatana na makohozi mazito.

Dk Mandai anasema, ugonjwa mwingine ambao unaweza kutibiwa na kiungo hicho ni kuharisha, hali kadhalika pia husadia kutibumishipa iliyovimba ambayo hujikunja na hivyo kusababisha maumivu makali sana na mara nyingine mishipa hiyo huonekata katika miguu ya watu wa makamo na akina mama wajawazito.

Pia Dk Mandai anasema, kitunguu swaumu ni tiba nzuri ya magonjwa ya ngozi yenye vilenge lenge (ecsema), ambapo dalili zake ni madoa meupe yenye magamba (huchunika kama ngozi iliyoungua) mikononi, miguuni, shingoni au usoni kote hutibiwa pia kwa kutumia kitunguu swaumu.

Kitunguu swaumu pia hutibu aina mbalimbali za tambaza kama ya mifu, misuli na viungo pamoja na wale watu wenye matatizo ya kupata choo kwa muda wa siku mbili au zaidi anaweza kutibiwa kwa kutumia kitunguu swaumu.

Aidha, pia inasaidia shida ya pumu na kubanwa katika mapafu pamoja na kushindwa kupumua ghafla, hali kadhalika hata ukiumwa na ng’e unaweza kusaga kitunguu kisha bandika pale ulipoumwa.

Hizo ni miongoni mwa faida za kitunguu swaumu, lakini unaweza kutembelea kituo cha Mandai Hrbalist Clinic kilichopo Ukonga, Mongolandege kwa ajili ya kupata tiba halisi za mimea. Pia kama wewe ni unapenda kusoma makala  za namna hii zinazohusu mimea na matunda ambayo ni tiba basi utaweza kuzipata nyingi sana kwa kutembelea www.dkmandai.com 

1 comment:

  1. Habari Mkusanyiko: Kama Ulikuwa Hujui Kuwa Kitunguu Swaumu Ni Dawa Fanya Ukutane Na Dk Mandai Hapa Akieleza Zaidi >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Habari Mkusanyiko: Kama Ulikuwa Hujui Kuwa Kitunguu Swaumu Ni Dawa Fanya Ukutane Na Dk Mandai Hapa Akieleza Zaidi >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Habari Mkusanyiko: Kama Ulikuwa Hujui Kuwa Kitunguu Swaumu Ni Dawa Fanya Ukutane Na Dk Mandai Hapa Akieleza Zaidi >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK

    ReplyDelete

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname