TOTO AFRICAN YAICHAPA MABAO 2-1 TIMU YA POLISI YA TABORA



Timu ya Polisi Tabora jana imeshindwa kuonesha umahiri wao baada ya kupokea kipigo cha Mabao 2-1 dhidi ya Toto African, mchezo ambao ni Ligi daraja la kwanza.



Mchezo huo ambao ulichezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza , ambapo Polisi ilianza kujipatia bao la kwanza katika dakika ya 18 na Hamis Twala likifungwa kwa njia ya penalt.

Kipigo hicho kilianza kupoteza matumaini kwa Toto, ambapo mpaka kumalizika kwa kipindi cha kwanza Toto haikuweza kuonesha ubabe kwa Polisi.

Lakini baada ya kuingia kipindi cha pili mchezo uliendelea vizuri na katika kuelekea ukingoni mwa mchezo huo katika dakika za nyongeza Timu ya Toto ilianza kujipatia magoli mawili mfululizo, huku yakifungwa na James Magafu katika dakika ya 93 na Jafari Mohamed dakika ya 94.

Mbali na hayo, hali ilibadilika ghafla uwanjani pale muamuzi wa mchezo huo Jamada Amada baada ya kupokea kipigo hadharani kutoka kwa Timu ya Polisi kwa kile kilichodaiwa kupendelea upande mmoja hali iliyopelekea Jeshi la Polisi kuingilia kati ili kutuliza ghasia hizo kwa kupiga risasi hewani.

Naye Kocha wa Polisi Tabora, Kim Christopha, akizungumza baada ya mechi kumalizika, alikiri kuwa Timu ya Toto imeshinda kihalali na wamekubaliana na matokeo, lakini alisema kuwa anailaumu TFF kutokuweka ulinzi wa kutosha katika mechi kubwa kama hizo ambazo zinahudhuriwa na watu wengi wenye nia tofauti tofauti.

Kwa upande wake Kocha wa Toto, John Tegete alisema juhudi za wachezaji wake na kujituma zimefanya wakashinda japo mchezo ulianza kuharibika kuanzia hapo awali.

‘’ Siri ya ushindi ni kujituma na hii imejidhihirisha wazi leo kwa vijana wangu sio kama Polisi Tabora walivyoanza kujiangusha angusha ili kupoteza muda, lakinI ushindi ni wetu,’’ alisema Tegete.

Naye Mwenyekiti wa Toto Waziri Gao alisema kumekuwa na tabia hii ya timu za kipolisi kufanya fujo ambayo ni makosa ya TFF kutangaza kuwa timu hizo zitashuka.


‘’ TFF imefanya makosa kutangaza mapema kuwashusha hawa, lakini sisi hatuogopi kitu sisi nia yetu ni kuongoza ligi na sasa tumerudia katika kiti chetu ambacho kinapaswa kukaliwa na sisi’’ alisema Gao.
Taarifa hii imeandaliwa na Goodluck Ngowi, mwakilishi wa habarimkusanyiko.blogspot.com kutoka jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname