MAKANISA YACHOMWA NIGER KATIKA MAANDAMANO



Makanisa mawili yamechomwa katika mji mkuu wa Niger, Niamey hii leo wakati wa maandamano ya kupinga kuchorwa kwa kiragosi cha mtume Muhammad katika jarida la Ufaransa la Cahrlie Hebdo wiki hii.


Kiasi ya askari 100 wa kutuliza ghasia walishika doria nje ya kanisa kubwa mjini Niamey kulilinda dhidi ya ghadhabu za waandamanaji, ambapo waislamu walikuwa wakirusha mawe.Mapema.

Aidha, polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kwa waandamanaji zaidi ya 1,000 gesi ili kuwatawanya nje ya msikiti mkubwa mjini humo huku ghasia zikiripotiwa pia viungani mwa mji huo mkuu.

Kufuatia tukio hilo ubalozi wa Ufaransa nchini Niger umewashauri raia wake walioko mjini humo kusalia majumbani baada ya waandamanaji hao kupora biashara kadhaa zinazomilikiwa na Wafaransa.

Lakini pia itakumbukwa kwamba maandamano hayo yanakuja siku moja baada ya polisi na raia watatu kuuawa katika maandamano ya kupinga kuchapishwa jarida hilo la Chalie Hebdo likiwa na picha za kikaragosi cha mtume Muhammad.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname