LULU:SITAFANYA KAZI NYINGINE ZAIDI YA FANI YA KUIGIZA



Star wa filamu hapa bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya.


Imekuwa ni kawaida kwa wasanii wengi hapa nchini kujihusisha na sanaa pamoja na shughuli zao nyingine kwa lengo la kujipatia kipato, lakini kwa msanii huyu amesema kamwe yeye hatakuja kufanya hivyo.

Hayo aliyasema alipokuwa akizungumza na mwandishi wa GPL, ambapo Lulu alisema, amegundua kuwa kila kitu kinatakiwa kifanywe kama kazi na yeye atakuwa akifanya kazi yake ya kuigiza tu na si vinginevyo.

“Napenda kuwa msanii na ninaamini mimi ni msanii, niweke wazi kwamba mimi katika maisha yangu sitarajii kuja kuwa dairekta au script writer wala kuja kufanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kuigiza”
Aidha Lulu aliendelea kusema kwamba “asilimia kubwa ya wasanii hapa kwetu hatuwazi mbali, chochote tunachofanya tunaona ni sawa tu hatupo kibiashara kwa sababu bado ni masikini ndiyo maana wengine wanaigiza ili waonekane, tubadilike.”
Asante kwa kutembelea blog hii, tafadhali endelea kuwa nasi 

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname