WEMA AJUTIA KUTOKA KWA UJAUZITO WAKE


IMEELEZWA kuwa mrembo na mwigizaji wa filamu, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ anadaiwa kujutia mimba yake aliyopachikwa na aliyekuwa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba ‘The Great’ wakati wa mapenzi yao.


Taarifa kutoka katika chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo Wema kilieleza kwamba, mwanadada huyo kwa sasa yupo kwenye wakati mgumu na akijutia mimba aliyopewa na Kanumba ambayo ilitoka kwa bahati mbaya, huku akibainisha kwamba huyo ndiye alikuwa mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito.

“Yaani Wema anajutia kweli kwamba kwa nini hakuzaa na Kanumba kwani ndiye mwanaume pekee aliyewahi kumpa ujauzito ambapo kwa sasa anatafuta mtoto lakini hapati, yaani yupo kwenye wakati mgumu sana akikuelezea mwenyewe unaweza kulia kwani ana simulizi ya kusikitisha kuhusu maisha yake na Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.


Hata hivyo chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa “hii yote inatokana na kwamba kwa sasa anatamani kuitwa mama lakini hapati hivyo kujikuta akiukumbuka ule ujauzito wa Kanumba anateseka kweli moyoni,”
Taarifa zinaeleza kuwa alipoulizwa Wema kuhusu suala hilo alikiri na kuonesha namna gani anateseka moyoni.

“Nateseka kweli, tangu ilipotokea kwa Kanumba haijawahi kutokea tena. Hakuna mtu ambaye hapendi kuwa mama, nazidi kumuomba Mungu huenda na mimi itatokea nitapata,” alisema Wema.
Source: Bongomovies.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname