WAKATI VIJANA WAKIKIMBIA MIMBA WALIZOWAPA MABINTI MITAANI, H.BABA ANASEMA MIMBA YA MKE WAKE NI MAFANIKIO



Mara nyingi kila mwaka unapoanza watu wengi hupanga mipango yao ili kuhakikisha mwishoni mwa mwaka wanakuwa wamefikia malengo waliojiwekea, na kuhusu suala la kupanga mipango hiyo ya mwaka mzima hapo ni kila mtu huwa na vipaumbele vyake, lakini kwa mwaka jana msanii wa kizazi kipya H.Baba yeye anasema kitendo cha mke wake kupata ujauzito ni moja ya hatua ya mafanikio kwake.


Hayo yanafuatiwa baada ya mke wa msanii huyo, ambaye pia ni mwigizaji wa filamu hapa nchini Flora Mvungi, kuwa katika matarajia ya kujifungua mtoto wa pili hivi karibuni.

H. Baba aliyathibitisha hayo kupitia 255 ya XXL, ambapo alisema kuwa mke wake Flora Mvungi ni mjamzito na hivyo wanatarajia kupata mtoto wa pili, huku akisema kuwa yeye kwake anaamini hali hiyo kwa mke wake ni miongoni mwa sehemu ya mafanikio aliyoyapata mwaka jana.
Muigizaji wa filamu Flora Mvungi ambaye anataraji kupata mtoto wa pili
“Faida ya mwaka jana ni mwana mama Flora Mvungi kujaa tena,” alisema. “Nikwambie kitu kimoja mimba huwa haipigiwi kelele, wala mimba sio kwenye magazeti. Mimi mimba huwa inaonekana, nawafundisha vijana wenzangu mimba sio kelele kwenye magazeti wala kwenye media hapana na mimba inaonekana baba. Flora Mvungi ameonekana kwahiyo ana mimba tayari. Kwahiyo nawafundisha vijana wenzangu ukicheza mechi vizuri utapata matokeo mazuri.” alisema H.Baba

Ni mara kadhaa mwana mama huyo Flora amekuwa akiweka picha kadhaa mtandaoni akionekana “amejaaa.”
Asante kwa kuendelea kuwa nasi kupitia habarimkusanyiko.blogspot.com, tunathamini uwepo wako msomaji wetu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname