WANANCHI WA KANDA YA ZIWA WANATARAJIWA KUANZA KUNUFAIKA NA USAFIRI WA KIVUKO




Wananchi wa vijiji vya Ilunda na Nyalwambu kata ya Ngoma wilayani Sengerema mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika na huduma ya usafiri baada ya Kivuko cha Mv Temesa, kuanza safari zake kutokea katikati ya jiji hilo mpaka vijijini kwao.



Hayo yalisemwa na hivi karibuni na Kaimu Meneja Wakala wa ufundi na Umeme (TEMESA) , Mhandisi Ferdinand Mishamo wakati akizungumza na wanahabari
ofisini kwake.

Mishamo alisema wameamua kuongeza idadi ya vituo katika usafirishaji abiria wa kivuko hicho, ili kuwarahisishia wananchi katika suala zima la usafiri kutoka katika vijiji na kwenda katikati ya jiji la Mwanza, kupitia ziwa Victoria, ambapo hapo kabla walikuwa na vituo vitatu ambavyo ni Luchelele, Sweya na Chakulabarafu, lakini kwa sasa wameongeza vituo vitatu ambavyo ni Ilunda, Nywalambu na Kirumba.

’Tumeamua kuongeza vituo hiyvo, ili kuwasaidia wananchi wavijiji vya Ilunda na Nywalambu katika suala zima la usafiri, hasa kipindi cha kusafirisha maziwa kupeleka katikati ya mji kwani walikua wanatumia mitubwi jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao” alisema Mishamo

Aidha, Mishamo alisema mwitikio wa watu kutoka vijiji hivyo viwili ni mkubwa kwani wengi wamekuwa wakisafirisha maziwa kutoka huko na kuleta mjini kwa ajili ya kuuza, hata hivyo alisema kwa upande wa watu wanaotoka wilaya ya Nyamagana bado hawajajua umuhimu wa kivuko hicho.

Mishamo aliendelea kusema mbali na mwitikio wa watu, bado wengi wao wanatumia usafiri wa mitumbwi, ambao ni hatari kwa maisha yao, kwani usafiri
huo siyo wa kisasa na hauna vifaa bora vya kuokolea endapo itatokea ajali.

Hata hivyo, Mishamo aliwaomba wananchi kukitumia kivuko hicho kwani kinafaida, pia kitawasaidia katika suala zima la usafiri, huku akisema kwamba kina
uwezo wa kubeba abiria wengi na mizigo kwa wakati mmoja na kuongeza kuwa pia vifaa vya kisasa ambavyo hutumika katika kujiokolea kama ajali itatokea.
Shukrani za pekee kwako kwa kuamua kutembelea blog hii, tafadhali tunakusihi endelea kutuunga mkono msomaji wetu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname