FAHAMU ALICHOKISEMA MUIGIZAJI WA FILAMU NCHINI KUHUSU WALE AMBAO HUSIFU WATU KWA KUWAPONDA WENGINE





Muigizaji wa filamu za kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewashukia wale ambao husifu wengine kwa njia ya kuwakosoa wengine.
Katika suala hili Lulu alisema kwamba
“niongee kidogo kuhusu hili kwa wanawake na wanaume....hivi kuna baadhi ya watu mnashindwa kabisa kumsifia mtu bila kuponda wengine....!?? Au kupenda mtu bila kuchukia wengine...!? alihoji msanii huyo.
Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu'
Staa huyo aliendelea kusema kwamba “kwa ufupi tu iko hivi....Kila mwanamke duniani ana uzuri wake na ana kitu ambacho mwanamke mwingine hana, hata wanaume pia...!”

Mbali na hayo, mrembo huyo aliongeza kuwa kuna watu fulani hawawezi kabisa kumsifia mtu bila kumponda mwingine, inafurahisha sana kutaka kulazimisha kuwa Mungu, huku akisema hivi unafikiri Mungu alikuwa hayuko sawa kufanya wanawake wawe wengi tena wengi zaidi ya wanaume, we fikiria tu na utulize akili yako ya kipuuzi.....!!!
Sambamaba na hayo Lulu alisema “hapa duniani ukiona unataka kuwa peke yako au kusifia mtu kwa kuponda wengine ni bora ufanye maombi Mungu akupeleke au ampeleke mtu wako sayari ya tofauti na dunia kama Jupiter huko au Pluto maana duniani ndo tumeshajazwa hivyo.
maneno yamekuwa mengi, lakini maana yangu ni hii hakuna haja ya kumsifia mtu kwa kuponda wengine au kumpenda mtu kwa kuchukia wengine”
Lulu alimaliza.

Shukrani kwa kuendelea kutembelea blog hii, tafadhali endelea kuwa nasi

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname