JB:MWAKA HUU NIMELENGA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA WAPYA ZAIDI


Mwigizaji na mwongozaji wa filamu hapa bongo, Jacob Stephen ‘JB’ ambaye pia ni Mkurugenzi na mliliki wa kampuni ya maswala ya filamu ya Jerusalem amesema kuwa katika mwaka huu amelenga zaidi kuibua vipaji vipya vya waigizaji hapa nchini hususani wale wa mikoani.



JB amesema kwamba yeye katika mwaka huu atacheza filamu mbili tu, lakini atakuwa akiandaa filamu nyingi ambazo atawaachia watu wengine waonekane hasa kutoka Zanzibar, Mwanza, Arusha, Dodoma pamoja na Mbeya.

Aidha, staa huyo katika tasnia ya bongo movie alisema kwamba “tutazalisha mastaa wengi kama tulivyofanya kwenye ‘Bado Natafuta,‘Wageni Wangu’ pamoja na ‘Chausiku” na mwisho alimalizia kwa kusema "Jerusalem ni yenu vijana"

Na katika kulidhibitisha hilo kwa vitendo JB alitupia moja ya picha inayoonesha miongoni mwa scene zitakazoonekana katika filamu aliyoitaja kwa jina la ‘Mzee wa Swaga’ na kuandika kuwa “Mzee huyo mwenye kofia anaitwa Chimbeni Herry, hii ni moja kati ya scene utakazo ziona ndani ya mzee wa swaga. Hapo ni Zanzibar, kati ya wasanii wazuri ambao hawajatumika vizuri ni pamoja na huyu” 

Picha ya scene hiyo ni hii hapa chini
Aidha, JB akimzungumzia zaidi mzee Chimbeni Herry alisema maneno haya “jamaa anaweza”

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname