KIONGOZI WA MTANDAO WA UJAMBAZI KATIKA MIKOA YA KANDA YA ZIWA AKAMATWA


MAKAMANDA wa polisi mikoa ya Simiyu, Mwanza na Shinyanga wameshirikiana katika mbinu mpya ya kudhibiti matukio ya uharifu ukiwemo yakiwemo yale ya ujambazi wa kutumia silaha pamoja na mambo mengine na hatimaye makamanda hao wakakutana kuwataja wahusika wa matukio hayo katika mikoa hiyo.


Katika zoezi la kuwataja wahusika wa matukio hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola, alimtaja kiongozi mkuu wa mtandao wa ujambazi katika mikoa ya kanda ya ziwa ambaye ni Njile Samweli (46) mfanyabiashara wa mjini Bariadi Mkoani Simiyu.

Kamanda Mlowola, alisema polisi ilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Januari 5 mwaka huu saa 13.00 baada ya kukwepa mkono wa dola kwa muda mrefu na kwamba alikuwa akianzisha mtandao wa kutekeleza matukio ya kiuarifu katika sehemu mbalimbali.

“Bwana Njile alikuwa anaanzisha mtandao mmoja na baada ya muda huwauwa washiriki wake nakutengeneza mtandao mwingine, hivyo mbinu hii ilimsaidia kukwepa wapelelezi,” alibainisha kamanda.

Makamanda wa Polisi wakizungumza na wanahabari, Valentino Mlowola Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo-Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu
na Justus Kamugisha-Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga.
Aidha, Kamanda Mlowola alielezea mbinu waliotumia kumkamata mtuhumiwa huyo kwamba walifanikiwa kumkamata mmoja wapo wa mtandao huo Mabula Lyagwa (36) mkazi wa Maswa ambaye aliponea chupuchupu kuuwawa baada ya kupigwa risasi kwenye bega lake la kulia na Njile.

“Baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema Bwana Lyagwa alihojiwa na polisi na kueleza kwamba jeraha hilo alipigwa risasi na jamabazi mwenzake aitwae Njile wakati wakifanya ujambazi kijiji cha Idukilo kata ya mwadui Mkoani Shinyanga” alieleza Mlowola.

Hata hivyo, kamanda alisema kufuatia maelezo ya wapelelezi kutoka Mkoani Mwanza walielekea Simiyu huku wakiwa na mtuhumiwa Lyagwa ambako waliungana na askari wengine hivyo kuanzisha msako wa kumtafuta mtuhumiwa na ndipo walifanikiwa kumkamata mhusika Njile ingawa hakueleza wazi kitu gani
alichokuwa akifanya wakati wanamkamata.
Habari hii imeandaliwa na Goodluck Ngowi, ambaye ni mwakilishi wa blog hii kutoka jijini Mwanza, asante sana msomaji wetu kwa kuendelea kufuatilia taarifa zetu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname