WATANZANIA WATAKIWA KUWA NA IMANI NA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI


Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju amewataka Watanzania kuwa na imani na Serikali iliyopo madarakani, lakini pia amewataka kumpa muda kabla ya kuanza kuipitia mikataba yote inayodaiwa kuwa na utata ili aweze kutoa ufafanuzi wa kina.

Lakini pia Masaju amesema kwamba, hadhani kama watu wanaosema kuwa baadhi ya mikataba iliyoingiwa na Serikali ina utata wako sahihi.

“Watu wanasema hivyo ila kuna jambo moja ambalo wanatakiwa kujua kuwa kuna baadhi ya mikataba ambayo ni siri,” alisema.

Masaju aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki ili kuchukua nafasi ya Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow. Kabla ya uteuzi huo, Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kuhusu uteuzi wake, alisema; “Nina furaha kwa sababu ninalitumikia Taifa na kuteuliwa kwangu kunaonesha kuwa Serikali ina imani na mimi.”
Hata hivyo, Masaju licha ya kubanwa na waandishi wa habari kuwa kwa nafasi aliyokuwa nayo hapo awali anafahamu maeneo yenye matatizo, ikiwamo na mikataba yenye utata, alisisitiza kuwa apewe muda zaidi.

Itakumbukwa kwamba Jaji Werema aliomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusu suala hilo haukueleweka na badala yake kuchafua hali ya hewa.

Asante kwa kuendelea kuungana nasi kupitia habarimkusanyiko.blogspot.com tunaahidi kuendelea kuwa pamoja mwaka huu 2015 katika kupashana habari katika nyanja zote

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname