KUTANA NA UKWELI KUHUSU MAHUSIANO KATI YA LULU NA IDRIS



Mshindi wa Shindano la Big Brother Hotshots 2014, Idris Rashid Sultan amefunguka kuhusu mahusiano yake na mwigizaji Elizabeth Michael ‘lulu’ ambapo Idris amesema amejuana na Lulu na kuwa marafiki na kupitia kazi yake ya kupiga picha na kusanifu kurasa za majarida.

Hayo aliyasema alipokuwa akizungumza na Global TV, ambapo kuhusu kuwepo kwa uhusiano na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ Idris alisema kuwa “mimi ni mpiga picha na msanifu kurasa, Lulu alikuwa anakuja nampiga picha na ni rafiki ambaye tumejuana kwenye kazi tu, sitaki kujua amejiwekaje”
Mbali na hayo, Idris alizungumzia ndoto zake za kufanya kazi Hollywood ambapo alisema anaamimi ana kipaji kikubwa cha kuigiza japo kuwa kwenye jumba la Big Brother alionesha kipaji cha kucheza.

“Nina ndoto kubwa ya kufika huko, nilivyofika kwenye ile nyumba nilikuwa nina kipaji cha kucheza lakini pia naamini niko vizuri kwenye uigizaji hata kutoka kwa Fig, Big, washiriki wenzangu, mwalimu mwenyewe anashangaa kwa hiyo ninahitaji kuendeleza hicho kitu” alisema Idris.





Endelea kuwa nasi katika kupashana habari kupitia kwetu habarimkusanyiko.blogspot.com, tunashukuru kwa kutembelea blog hii.


No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname