WATU ZAIDI YA 50 WAFARIKI BAADA YA KUNYWA POMBE


Watu 50 wamepoteza maisha baada ya kunywa kilevi kinachoelezwa kuwa na sumu. Watu hao walikunywa kilevi hicho walipokuwa msibani.

Tukio hilo lilitokea siku ya Jumamosi na taarifa zinaeleza kuwa mbali na watu 50 kufariki, watu wengine kadhaa waliokunywa kinywaji hicho walikimbizwa hospitalini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa maafisa wanasema wanaamini kuwa kilevi hicho cha kienyeji, kinachoelezwa kutengenezwa kwa kutumia mtama na mahindi kilikuwa na sumu ya nyongo ya mamba wakati waombolezaji walipokuwa makaburini.

Hadi sasa sampuli za damu za watu walioathirika na pombe hiyo pamoja na sampuli za bia tayari zimepelekwa mji mkuu wa nchi hiyo, Maputo kwa ajili ya uchunguzi.


Taarifa mbaya zaidi ni kwamba hata mwanamke aliyetengeneza pombe hiyo sambamba na nduguze ni miongoni mwa waliopoteza maisha.

Kufuatia tukio hilo Serikali ya Msumbiji imetangaza siku tatu za maombolezo nchi nzima, huku uchunguzi kuhusu tukio hilo ukifanyika.
Shukrani za dhati kwa kuamua kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com na kutufanya kuwa chanzo chako cha kupata habari, tafadhali endelea kuwa nasi.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname