DIAMOND AANZA SHOPPING KWA AJILI YA MWANAYE MTARAJIWA


Mwanamziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema ameanza kufanya manunuzi kwa ajili ya mtoto wake anayetarajiwa kuzaliwa hivi karibuni.


Hayo yalibainika kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliweka picha mbalimbali zinazoonesha toi za kuchezea watoto pamoja na magari.

“Ushambaa huu…eti nimeshaanza kununua vitoi vya kucheze mtoto, Mungu anisaidie mwanangu azaliwe salama jamani” aliandika staa huyo.

Taarifa zinasema kuwa staa huyo yupo Zanzibar kwa ajili ya mapumziko akiwa na mpenzi wake , Mganda Zarina ‘Zari Boss Lady’
Asante kwa kuendelea kutembelea blog hii.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname