'JB' AMKUMBUSHA RAIS KIKWETE KUTIMIZA AHADI YAKE


Mwigizaji nguli na muongozaji wa filamu za Kibongo, Jacob Steven ‘JB’, amesema kuwa, licha ya kuendelea kulia juu ya kuibiwa kazi zao, lakini bado rais hajatimiza ahadi yake kwenye tasnia hiyo.

Staa huyo wa filamu nchini alisema kuwa anamkumbusha Rais Jakaya Kikwete kutimiza ahadi yake aliyowahi kusema kwenye msiba wa nguli wa filamu, Steven Kanumba kuwa atawashughulikia wale wote wanaoiba kazi za wasanii na kutoa kopi.

JB alitoa ombi kwa uchungu ambapo alifunguka kuwa pamoja na kuwepo kwa wasambazaji, lakini bado wasanii wamekuwa wakilia kila siku hasa pale wanapopeleka filamu zao sokoni.

“Rais wetu alitoa kauli kuwa anawashungulikia wale wote wanaohusika na wizi wa kazi zetu, lakini hadi leo bado hajatekeleza hilo, lakini hatuwezi kushindwa kusema kuwa tunaumia sana, tunaomba atusaidie,” alisema JB.


Shukrani za pekee kwa kuendelea kuichagua blog hii kwa kujipatia habari mbalimbali, tafadhali endela kutuunga mkono na kama unatukio lolote au tangazo usisite kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716514718 email habarimkusanyiko@gmail.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname