KAULI ZA MASTAA KUHUSU MATUKIO YA MAUAJI YA ALBINO HAPA NCHINI


Kufuatia kuendelea kwa matukio ya mauaji na ukatili kwa Watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi (albino) hiki ndicho walichokiandika mastaa mbalimbali hapa nchini kupitia mitandao ya kijamii.

Riyama Ally
“Kiukweli siwezi kulala leo bila kusema haya nitakayosema.. hawa ni wenzetu na wanastahili tabasamu zaidi ya wanalolitoa wenyewe wanahitaji mapenzi yetu ya ziada.. lakini wapi binaadamu wenye uchu na tamaa za madaraka, pesa, biashara kukua haraka na mengi mengineyo wameupa kisogo utu na kuondoa japo kwa uchache tabasamu dogo walilonalo... tunakwenda wapi jamani kwa kukata viungo vya wenzetu... nani wa kumlaumu wa kwanza ni wewe mwenye tamaa ya madaraka..pesa.. whatever.. lakini pili mganga wako aliyekudanganya ukalete kiungo hicho ili ufanikiwe.. nyie wote na mungu anawaona adhabu dhidi yenu wala hajaisahau hajalala mungu...na anawaona inshallah.. poleni ndugu zetu mlioathirika kwa namna moja au nyingine kwa janga ili.. mungu ibariji africa mungu ibariki tz tupe roho za imani inshallah.. amen. Plz piga vita mauaji ya albono kwa pamoja tunaweza....”.



Shamsa Ford
“Yaani hata sijui nisemeje maana kila nikifikilia mwanadamu anayefanya ukatili huu wa kuwaua walemavu wa ngozi naumia sana.kikubwa naomba Mungu wote wanaohusika na huu unyama wakamatwe.. inshaallah Mwenyezi Mungu atasimamia kwa hili”.
Kitale
Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.
Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.
Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.
Wanaoniunga mkono mikono juu, dah! Aiseee naomba mm niwe wa kwanza kukuunga mkono mdimuz

Batuli

Kila ninachoandika machozi yananitoka, I'm speechless, Nadhani kupost insta haitoshi tunahitaji maandamano ya mkoa kwa mkoa kutetea haki za wenzetu, Tunahitaji kujitoa zaidi kuwasaidia watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi, Tunahitaji nguvu zaidi, Mungu simamia haki za viumbe hawa hukuwaumba kimakosa...stopalbinokillings ..stopalbinokillings ..stopalbinokillings

Hemedy PHD

Imani zisizompendeza Mungu ndio hupelekea baadhi ya watu kufanya unyama wa kikatili kiasi hiki...hawa ni binadamu kama wewe na wana haki ya kuishi kwa amani na upendo..poleni kwa wote mliopatwa na matatizo haya!..MUNGU ATAWASIMAMIA INSHALLAH!...STOP KILLING ALBINO! ..VERY DISAPPOINTED

Maneno kutoka kwetu habarimkusanyiko blog:Matukio haya yanaumiza sana kwa kweli na ni dhambi kubwa ambayo hapo baadaye tusipokuwa makini damu hizi zinazopotea zitakuwa zikiendelea kulililia taifa hili na kujikuta tukiendelea kukubwa na majanga mbalimbali hapa nchini yakiwemo mafuriko, ukame, njaa na hata vita, hivyo ni vizuri kila mtu katika taifa hili akasimama kwa nafasi yake kupinga mauaji ya ndugu zetu hawa walemavu wa ngozi.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname