RICHI MAVOKO: VIDEO YA PACHA WANGU IMENIFUNGULIA MILANGO

Msanii wa bongo fleva Rich Mavoko amesema kuwa kufuatia video yake ya pacha wangu imemsaidia kufungua milango mingine.

Msanii huyo ambaye kupitia video yake hiyo amepata dili la kuwa balozi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali linalojishughulisha na uhifadhi wa mazingira na wanyama pori liitwalo 'World Wide Fund for Nature' (WWF).

Akizungumza jijini Dar es Salaam msanii huyo alisema dili hilo amelipata kutokana na video yake ya pacha wangu aliyoirekodi nchini Afrika Kusini ambayo ndani yake amemtumia mnyama chui.

Rich Mavoko alisema "baada ya kuiangalia video ya pacha wangu waliipenda na kuamua kufanya kazi na mimi"

Pamoja na hayo, Mavoko alibainisha kuwa shirika hilo lilipenda kufanya kazi naye kwa lengo la kuwashawishi vijana wengine kutunza mazingira.

Asante kwa kuendelea kutembelea blog hii.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname