STAA WA MZIKI WA BONGO FLEVA MEZ B AFARIKI DUNIA

Miongoni mwa taarifa za kusikitisha hii leo Februari 20 ni kuhusiana na hii taarifa ya kifo cha msanii wa muziki wa bongo fleva Mez B.

Taarifa kutoka kwa dada wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Rachel amethibitisha kutokea kwa kifo cha msanii huyo alipokuwa akizungumza na moja ya kituo cha redio hapa nchini na kusema kuwa kifo hicho kimetokea nyumbani kwao Dodoma.

Aidha, taarifa zaidi zinasema kuwa msanii Mez B alikuwa akisumbuliwa na homa tangu mwezi Disemba mwaka jana.

Msiba uko nyumbani kwao eneo la kisasa, Dodoma

Hii ni video ya mwisho iliyofanywa na Mez B enzi za uhai wake.



Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname